Friday, January 17, 2014

AMA KWELI WALIMWENGU HAWANA HURUMA:WATOTO WAWILI WA KIKE WABAKWA

WIMBI la ubakaji wa watoto wadogo limeendelea, baada ya watu wawili kuripotiwa kuwabaka wasichana wadogo wa kike katika matukio mawili tofauti wiki iliyopita.



Mtoto aliyebakwa.
Huko Mbagala Zakhem, jijini Dar, kijana aliyefahamika kwa jina moja la Robert alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka tisa baada ya kumnywesha bia na baadaye kumchoma kwa kisu chenye moto katika harakati za kulazimisha kitendo hicho.
Mama mzazi wa msichana huyo, Neema Mohamed, aliliambia gazeti hili kuwa Alhamis iliyopita mtoto wake hakurudi nyumbani baada ya kuondoka na msichana aitwaye Anna, ambaye ni jirani yao aliyemuomba mapema amsindikize saluni kwa ajili ya kusuka.
“Nilihangaika sana kumsaka mwanangu, yule dada akawa anakataa kwamba hajui alipo wakati yeye ndiye aliondoka naye, nikatoa taarifa Kituo cha Polisi cha Mbagala Maturubai, juhudi zikazaa matunda kwa kumpata mwanangu na mtuhumiwa. Anna alipanga njama na Robert,” alisema.

Mtoto huyu naye alibakwa.
Mtoto Neema naye alikiri kufanyiwa unyama huo usiku wa manane na watuhumiwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Mbagala Maturubai kwa hati yenye kumbukumbu MBL/RB/426/2014, KUBAKA.
Wakati huo huo, mtoto mwingine aitwaye Prisca ambaye pia ana umri wa miaka tisa, mkazi wa Kongowe Mzinga mkoani Pwani, naye alifanyiwa unyama kama huo na mtu mmoja mwenye umri wa miaka 46 anayefahamika maeneo hayo kama Anko.
Mama wa mtoto huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema awali hakuwa akifahamu chochote hadi pale alipoelezwa na marafiki wa binti yake huyo kuhusiana na tukio hilo lililotokea Desemba mwaka jana.
Prisca aliliambia gazeti hili kuwa siku ya tukio, alipita jirani na nyumba ya Anko huyo aliyemuita na kumtuma vocha dukani, lakini aliporejea na kuingia sebuleni akabakwa
Mtuhumiwa huyo anatafutwa na jeshi la polisi kwa jalada la kesi MBL/RB/14111/2013 KUBAKA.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →