Ingekuwa ni msanii mwingine ungesikia ameshapotea katika ramani hii
ya muziki kutokana na ukimya wake ila siyo Ali kiba,akiwa ndiye nominee
wa tuzo za KORA 2012,mwaka jana ni mwaka ambao msani huyu aliweza kukaa
kimya kwa muda mrefu huku
watu wengi wakihisi kuwa ameacha muziki kabisa,ila si hivyo,Kati ya
wasanii wa hapa Bongo wanaoheshimika sana basi Ali Kiba anapewa nafasi
ya kipekee kutokana n uwezo wake wa kuimba na kule kutokuwa na drama
nyingi za hapa na pale kama kawaida ya wasanii wengi wa muziki huu
wa Bongo hasa pale wanapopata umaarufu,kuongelea kuhusu Ali kiba
unaweza kusema ni mfano wa msanii wa Bongo fleva,ni moja ya msanii
ambaye nyimbo zake zimeweza kukaa muda mrefu bila kuisha ile ladha ya
muziki wake.
Mbali na ukimya alionao wa mwaka mzima wa jana,ila bado hata wasanii
wenzake wamekuwa wakimkubali sana,kutokana na uwezo mkubwa wa kuimba
aliokuwa nao,kwa wasanii wanaochipukia,alikiba amekuwa kama reference point,yani
wasanii wanangalia wafanye muziki ili wafike level kama zake Ali
Kiba,ikiwa ni pamoja na kuwa na ndoto zakufanya kazi na msanii
huyu.Mwishoni mwa mwaka jana msanii chipukizi Naylee alifunguka na
kusema kuwa nyimbo za Ali Kiba ndizo zilizomfanya aweze kupata moyo na
kuingia katika maswala haya ya muziki na kuwa na ndoto siku moja kufanya
kazi na Ali Kiba.huyu ni mmoja tu ya wasanii chipukizi mwenye ndoto za
kufanya kazi,hivyo mbali na kuwa kimya kwa muda Ali kiba bado amekuwa
kwenye ndoto ya kila msanii kutaka kufanya nae kazi.
Nyimbo za Ali Kiba,kutokana na wadau mbali mbali waishio nje ya
nchi,wanasema kuwa hupigwa sana huko nje ya nchi,moja ya nchi zinazopiga
sana nyimbo za ali kiba ni huko Muscat,Inasemekana ni msanii wa bongo
fleva anayesikilizwa kuliko msanii yeyote yule,hata kwa wale wasiojua
kiswahili wamekuwa wakisikiliza nyimbo zake,..unaweza kufananisha haya
yote na nyimbo za michael jackson
hivi leo,sidhani kama watu wengi wanaopenda nyimbo zake wanajua
kingereza,ila bado wanasikiliza na kuzicheza.Ukirudi hapa East Africa
ali kiba bado anacheza role kubwa kwenye list ya kila mmoja ya nyimbo
azipendazo,na huko nchini kenya mbali na kutotoa hit single kwa kipindi
cha muda mrefu,ni moja ya msanii anayeongoza kwa nyimbo zake kuwa
requested sana,hii yote inaonyesha kuwa bado nyimbo zake zinapendwa sana
na watu,haijalishi nyimbo ni ya mwaka gani.
Ni moja ya msanii aliyekuwa poa sana kusaidia wasanii wadogo
wanaochipukia na hivyo kuwa kioo cha msanii ambaye anajali sana na
kuheshimu kazi za mtu mwingine,ukiongelea ali kiba ni msanii ambaye yuko
social sana na ameweza kusaidia wasani wengi sana wanaochipukia
kimawazo na hata kufanya nao collabo katika nyimbo zao,imekuwa kawaida
sana kwa wasanii wakubwa baada ya kupata umaarufu kusahau walipotoka
kuwa wao pia mwanzo walikuwa chipukizi wakitafuta njia yakutokea kwa
kukataa kabisa kufanya collabo na wasanii wachanga,but kwa A