Watoto walioachwa na mama yao wakiwa wamelaa eneo la makutano ya barabara ya Zaramo na Jamhuri jijini Dar.
KATIKA hali ya kusikitisha kamera yetu mchana huu imenasa picha za
watoto waliosemekana kuwa mama yao aliwaacha na kwenda kuombaomba
katikati ya jiji la Dar es Salaam.Watoto hao walioonekana kuwa na njaa kali walikutwa katika eneo la makutano ya barabara ya Zaramo na Jamhuri jijini Dar.
Mpaka mwanahabari wetu anaondoka eneo la tukio mama huyo alikuwa bado hajarudi na haikujulikana atarudi saa ngapi.