Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni katika mahojiano maalumu, Chilo aliyejizolea heshima na umaarufu mkubwa katika fani hiyo, alikiri kuwa wasanii wengi wamekuwa wakijitenga na
wenzao wakati wa matatizo jambo ambalo linakera na kuumiza.
Msanii huyo alisema hakuna binadamu anayejua hatima ya maisha yake hapa duniani, hivyo ni vyema kuishi katika mwenendo ulio mzuri, kwani watu wote ni udongo na mavumbini watarejea.