WASANII wa filamu, Ruth Suka ‘Mainda’ na Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’ sasa wameonekana kujikita zaidi kwenye mafunzo ya kiroho baada ya hivi karibuni kunaswa kwenye kongamano la
ukombozi ndani ya Ukumbi wa Vatican City Sinza jijini Dar walipokwenda kuabudu.
Ruth Suka ‘Mainda’.
Wawili hao walinaswa wakiwa na nyuso za unyenyekevu huku wakionekana
kudhamiria kumrudia Mungu na walipoulizwa walisema walikuwa katika
kongamano hilo la mafunzo ya kiroho na Biblia kwa siku tatu.
Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’.
“Sisi tumempokea Yesu, tunawasihi wasanii wenzetu waachane na
ushirikina waje huku ambako kuna njia salama, hili ni kongamano ambalo
lina mafunzo mema na lina uwezo wa kumbadili mtu kutoka kwenye roho ya
kishetani na kuwa na roho safi,” alisema Thea.