Askari polisi akimuongoza mama wa watoto hao polisi
Askari wanaharakati wa dawati la mtandao wa jinsia kulia na kushoto wakiwa wamemkamata mama wa watoto hao tayari kwenda polisi |
Hapa wakiingia na mama huyo katika ofisi za dawati la jinsia mkoa wa Iringa |
Mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa
Iringa Atupele Mwambunda (kulia) akimhoji mama wa watoto hao Watende
Sanga kuhusiana na ukatili uliofanywa dhidi ya watoto wake.
.................................................................................................
WAKATI wanaharakati mbali mbali
wakiwemo wanaharakati wa mtandao wa kijinsia Tanzania
(TGNP) ,wanaharakati wa haki za binadam,WAMA kuendelea kukemea na
kuendelea kupinga vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia na uyanyasaji
wa wanawake na watoto hata kulifanya jeshi la jeshi
la polisi kuanzisha dawati maalum linaloshughulikia vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia ,baba wa kambo Mussa Mdetela aamua kuwatesa
kinyama watoto wake kwa kuwachoma moto miguu wakituhumiwa kuiba Tsh
10,000
Wakizungumza kwa shida na mtandao huu
watoto hao Baraka Rajab Mohamed anayesoma darasa la kwanza na Mood
Rajab Mohamed anayesoma darasa la sita walisema kuwa ilikuwa ni
siku ya tarehe 3 ambapo walichukua pesa hiyo kiasi cha Tsh 10,000 na
kwenda kununua chakula baada ya mama yao kushindwa kuwaandalia
chakula.
Hata hivyo Mood anayesoma darasa la
sita msingi Lugalo alisema kuwa siku ya tukio mdogo wake alikwenda
ndani na kuchukua kiasi hicho cha fedha na baada ya
muda walishirikiana katika matumizi .
Watoto hao ambao wanadai kuwa
baba yao mzazi Rajab Mohamed aliwaacha na sasa anaishi jijini Dar es
Salaam na wao wamekuwa wakiishi na baba yao mdogo huyo ambae mara
kwa mara amekuwa akiwaadhibu vikali.
Kwani walisema kuwa kutokana na mara
kwa mara kushinda bila kula ndipo siku hiyo walipoamua kuchukua
pesa hiyo ili kununua bagia na vitumbua ili kujikimu kwa njaa .
Hata hivyo walisema baada ya baba
yao kurudi kutoka katika shughuli zake na kubaini kuwa fedha hiyo
imechukuliwa ndipo alipowakamata na kuwafunga kamba na kuanza kuwatesa
kwa kichapo ili waweze kusema mtu aliyechukua pesa hiyo.
“Alitufunga kamba miguuni na mikononi
na kuanza kututesa kwa kutupiga na baada ya kuona hatusemi ndipo
alipochukua makaratasi ya naironi na kutufunga miguuni kisha kuchukua
kiberiti ,mafuta ya taa na kuwasha moto katika miguu yetu huku
akiendelea kutupiga na moto ukiwaka miguuni….wakati huo mama alikuwa
amekaa mlangoni akishangilia kuwa wapige sana mimi nimewachoka hawa
watoto heri wafe tu” walisema watoto hao
Atupele Mwambunda mkuu wa dawati la
jinsia mkoa wa Iringa ameuthibitishia mtandao huu juu ya tukio hilo
na kuwa kitendo hicho ni cha kinyama na kamwe hakitavumilika.
Alisema kuwa kuanzishwa kwa dawati
hilo ni kutaka kukomesha vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia
kama hivyo na kuwataka wazazi na jamii kuepuka kuchukua sheria
mkononi kwa kuwatesa watoto kama hao ambao
mwisho wa siku wanapoteza mwelekeo wa maisha.
Mwambunda alisema kuwa hadi sasa
wamefanikiwa kumkamata mama wa watoto hao Watende Sanga
huku mzazi mwenzake Mussa Mdetele bado anatafutwa na jeshi la polisi
ili kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwatesa watoto hao.
Huku mama wa watoto hao akidai kuwa
wakati baba yao mdogo akiwapiga watoto hao yeye hakujua
kinachotokea japo alikuwa na taarifa ya kupotea kwa pesa katika duka
na kuwa baada ya tukio hilo aliwanunulia dawa ili kuwatibu kinyemela
pamoja na kuwaombea ruhusa shuleni .
Pia mwanamke huyo aliomba kusamehewa kwa madai kuwa hakujua kama kushangilia wakati baba yao akiwatesa watoto hao ni kosa