Habari
za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa uongozi wa
Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa
nidhamu wa watangazaji hao.
Hata
hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao wamepigwa chini
kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds
FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke,
Dar.
Risasi
Mchanganyiko lilimvutia waya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa
Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo ambapo
alikiri.
“Ni
kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya
kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha
usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa.
“Hatutakuwa
nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya
hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na
sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu
zetu,” alisema Ruge bila kufafanua zaidi.
Alipoulizwa
ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema: “Nashindwa
kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao watangazaji kwa
sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati tukifikiria cha
kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana.”
>>Gazeti la Risasi/ GPL
>>Gazeti la Risasi/ GPL