Lesego Motsepe (Lettie Matabane), enzi za uhai wake
Mwaka 2011 Lettie aliwahi kujitangaza kuwa anaishi na Virusi vya Ukimwi
Aliyekuwa muigizaji maarufu katika Tamthilia ya Isidingo The Need ya Afrika Kusini, Lesego Motsepe maarufu zaidi kwa jina la Lettie Matabane, amefariki dunia nchini mwake Afrika Kusini mapema leo.
Lettie, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa katika tamthilia hiyo kuanzia mwaka 1998 hadi 2008 alipoamua kuondoka, alikuwa akiishi na virusi vya Ulimwi kwa zaidi ya miaka 15. Mwaka 2011, aliwashitua mashabiki wake baada ya kuwatangazia kuwa yeye ni muathirika wa ukimwi.
Hata hivyo wengi walimpongeza kwa kuwa na ujasiri wa kujitangaza hadharani, kwani kwa miaka mingi alikuwa akifanya kazi ya ubalozi wa mambo ya ukimwi.
Aliianza kazi hiyo ya ubalozi kabla hajaathirika na hata alipoathirika hakushituka sana ingawa hali hiyo ilibadili maisha yake kabisa.
Tamthilia ya Isidingo ni miongoni mwa tamthilia kongwe na maarufu nchini Tanzania ambayo imekuwa ikioneshwa na televisheni ya ITV kwa zaidi ya miaka kumi sasa bila kuchosha watazamaji wake.
Mungu ailaze roho yake mahala pema - AMEEN!