Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamanda Mkadam Khamis Mkadam akionesha
bastola iliyotumia katika uhalifu wa kumpora fedha mfanyabiashara
katika maeneo ya rahaleo Zanzibar ikiwa na risasi zake kamili, ilihusika
katika tukio hilo.
Kamanda
Mkadam akionesha moja ya Silaha aina ya SMG ambayo ilikuwa haina
magazine waliokuwa wakiitumia watuhumiwa wa uhalifu katika maeneo ya
Raha Leo na kuitupa katika eneo la msikiti wa Muembe Shauri wakati
wakikimbia.
Silaha zilizokamatwa na watuhumiwa wa ujambazi huo
Habari za mchana ndugu wanahabari,
Kamanda
Mkadam akiwaonesha waandishi moja ya silaha aina ya
Gobole,waliofanikiwa Jeshi la Polisi kumkamata mtuhumiwa wakati
akijiandaa kwenda kufanya uhalifu maeneo ya mtoni.
Waandishi
wa habari wakifuatilia taarifa inayotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mjini Magharibi Kamanda Mkadam Khamis Mkadam, kuhusiana na uhalifu
uliofanyika mwanzo mwa wiki hii katika maeneo ya Rahaleo na kumpora
fedha shilingi milioni kumi na moja katika tukio hilo na polisi
kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao, kwa ushirikiano wa Wananchi wa
kwahani. Picha na Othman Mapara
Tumewaita
ili kutoa taarifa kwa wananchi juu ya tukio ambalo limetokea ndani ya
Mkoa wetu ambalo kwa kiasi kikubwa linataka ufafanuzi kutokana na jinsi
linavyozungumzwa huko nje.
Siku ya tarehe 13/01/2014 majira saa 9:55 jioni hapo Rahaleo kwa Mchina Tambi palitokea tukio la unyangani wa kutumia silaha.
Tukio
hili lilitokea wakati Bw: SAID SEIF SALAMI 34, Riami wa RAHALEO
ambaye ni MFANYA BIASHARA wa vyakula anayefanyia biashara yake Kibanda
Maiti na anaishi mtaa wa RAHALEO alipofanyiwa unyanganyi huo.
Mfanya
biashara huyu alifunga biashara yake majira ya saa 9:45 jioni ya siku
hiyo ya tarehe 13/01/2014 na kuchukua pesa za mauzo ya kutwa jumla ya
T.sh 11,500,000/= ambazo alizifunga katika bahasha /mfuko wa kaki na
kuondoka nazo kuelekea nyumbani kwa kutumia gari yake no. Z. 128 EW
NISSAN Rangi ya silver.
Alipofika
maeneo ya Raha Leo Kwa Mchina Tambi ndipo gari moja yenye no. Z.866 EX
aina ya SCUDO ilipomzinga kwa mbele na ghafla aliona watu watatu
wametokezea wakiwa na silaha mbili, moja ikiwa ni bastola na nyengine ni
SMG.
Watu hao walimlazimisha kwa
usalama wake awape ule mfuko wenye pesa. Kwa kuhofia usalama wake alitoa pesa zote jumla ya T.SH 11,500,000/=
Majambazi hao baada ya kitendo hicho cha kuchukua hizo pesa walikimbilia kwenye gari yao.
Kitendo
hicho kilifanyika mbele ya watu ambao walianza kupiga kelele za mwizi!,
mwizi!, mwizi!, kelele ambazo zilimfanya dereva wa gari ya majambazi
kuondosha gari na kuwaacha wenzao watatu chini.
Wakati huo wananchi walipiga simu Polisi huku juhudi za ukamataji
zikiendelea.