Wednesday, January 22, 2014

UPDATES: WANAFUNZI WANNE WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE 35 KUJERUHIWA AJILINI MKOANI MTWARA LEO



Wanafunzi 4 wa Shule ya sekondari ya Sabodo iliyopo mkoani Mtwara,wamefariki huku wengine zaidi ya 35 wakmiwa wamejuruhiwa katika ajali iliyotokea iliyotokea mapema leo asubuhi baada ya wanafunzi hao kugongwa na gari walipokuwa katika mazoezi ya asubuhi (Mchakamchaka) shuleni hapo ambayo ipo Pembezoni mwa barabara kuku ya Mtwara ,Lindi kuelekea Dar es salaam.

Waliofariki katika ajali hiyo iliyowakuta wanafunzi hao wa Shule ya Sekondari ya Sabodo ni Ailat,Nasma na Hilda mmoja bado hajafahamika,Wote ni wanafunzi wa kidato cha kwanza na wametambulika kwa jina moja moja kwa kila mmoja..

Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Ligula,mkoani humo kwa ajili ya matibabu zaidi.

Habari kamili inawaijia hivi punde

na Michuzi Blog 

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →