Mgombea
wa kiti cha urais wa shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, Jerome
Champagne, amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa kutoa kadi ya chungwa
wakati wa mechi za soka, ili kuruhusu marefa wa mechi kuwaruhusu
wachezaji waliofanya madhambi kuondolewa uwanjani kwa muda.
Champagne
mwenye umri wa miaka 55 kutoka Ufaransa, aliyasema hayo siku ya
Jumatatu wakati alipoanzisha kampeni yake ya kumrithi rais wa FIFA Sepp
Blatter, kufuatia uchaguzi wa urais wa FIFA utakaofanyika mjini Zurich
Juni mwakani 2015.
Amesema
ikiwa atashinda atapendekeza vilabu vya soka kuadhibiwa ikiwa wachezaji
wake watahoji maamuzi ya refa na vile vile kuchunguza uwezekano wa
kutumia teknolojia kutatua maamuzi muhimu.
Miongoni
mwa mapendekezo mengine aliyoyasema ni kuthibiti idadi ya wachezaji wa
kigeni wanaosajiliwa na vilabu, kutangazwa kwa mshahara wa rais wa FIFA
na maafisa wengine wakuu.
Aidha
ameahidi kuwa atafutilia mbali sheria ya sasa inayotoa adhabu tatu kwa
mchezaji ambaye atafanya madhambi katika eneo la hatari.
Kwa
sheria ya sasa mchezaji yeyote anayefanya kosa katika eneo la hatari,
hupewa kadi nyekundu moja kwa moja na pia kupigwa marufuku ya kutocheza
mechi mbili zinazofuata.
Source:BBC