Afisa
Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Eng Jackson Midala akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) juu ya matukio mbalimbali ya shirika lake kwa
mwaka 2013 na mategemeo ya uboreshaji huduma kwa mwaka 2014.Kulia ni
Ofisa Uhusiano wa Dawasco,Everlasting Lyaro.
Shirika
la majisafi na majitaka Dar es salaam(DAWASCO) imesema inawadai wateja
sugu Tsh 40 bilioni huku ikiwataka kulipa madeni ili kunusuru utendaji
wa shirika.
Kauli
hiyo imekuja siku chache baada ya DAWASCO kukatiwa huduma ya umeme na
TANESCO kutokana na deni la sh 6.3.
Hayo yamesemwa na afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO, Eng Jackson Midala
alipokuwa anaongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki.
Alisema mamlaka hiyo imeshindwa kulipa kulipa deni hilo kwa wakati
kutokana na kuwadai wateja wake zikiwemo taasisi za serikali zaidi ya
bilion 40. Alisema deni hilo linahusisha baadhi ya taasisi za serikali na watu binafsi
“Kuna hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Jeshi la Wananchi wa Wanzania (JWTZ), Polisi na wengine wengi. Hatuwakatii
huduma kwa sababu ya madeni ila tunasisitiza kulipa madeni hayo ili na
sisi tuweze kulipa mzigo wa madeni mengine ya umeme” alisema Midala
Alisema “hivi karibuni mtambo wa ruvu juu uliharibika na mafundi wetu
walifanikiwa kuutengeneza, lakini siku ya jumamosi umeme wa TANESCO
ulikatwa kwasababu ya deni, jambo lililosababisha Maji kukatika tena
kwenye sehemu nyingi za jiji la Dar es salaam”
Pia midala alisema kuhusu hatua zinazoendelea kuwashughulikia wateja
wanaoiba Maji kwa njia za kuharibu mita kwamba mpaka sasa wamewakamata
watu 284 na kuwafikisha mahakamani.
Alisema
miongoni mwa watu hao, watatu walihukumiwa adhabu ya kifungo, watatu
kesi zilifutwa kwa kukosa ushahidi na wengine kesi zao zinaendelea.
Aliwataka
wateja kulipa Ankara zao kwa muda, lengo likiwa kuwezesha mamlaka hiyo
kujiendesha na kuendelea kuwapa huduma na pia kutoa taarifa za wizi wa
Maji na uharibifu wa miundo mbinu kupitia simu yake ya Mkononi
0779-090900.