Wakati
ambapo rais wa Ufaransa, Francois Hollande na First Lady, Valerie
Trierweiler wanahangaika kuuweka sawa uhusiano wao kufuatia tuhuma za
Hollande kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji Julie Gayet, ndoa ya
rais Barack Obama wa Marekani na Michelle nayo inadaiwa kuwa juu ya
mawe.
Yote
yalianza kwenye hafla ya kumbukumbu ya Nelson Mandela mwishoni mwa
mwaka jana pale ambapo zilisambaa picha zinazomuonesha Michelle
akionekana kukerwa na kitendo cha mumewe kupiga picha ya ‘selfie’ na
Waziri Mkuu wa Denmark Helle Thorning-Schmidt.
Na kama magazeti ya udaku ya Marekani yanasema ukweli, uhusiano wa wawili hao upo kwenye matatizo makubwa.
Katika
kichwa cha habari kisemacho: ‘Obama Divorce Bombshell’, gazeti la
National Enquirer linadai kuwa ndoa hiyo yenye miaka 21 imekuwa
ikikumbwa na ugomvi wa mara kwa mara ulioanzishwa na tukio hilo kwenye
hafla ya kumbukumbu ya Mandela na mbaya zaidi ni kuwa Michelle amegundua
kuwa walinzi wa Secret Service wamekuwa wakificha uzinzi unaofanywa na
Obama.
Ni madai ambayo ikulu ya White House imegoma kusema chochote.
Gazeti
hilo linadai kuwa Mrs Obama, amepanga kuwa pamoja na mumewe hadi
atakapomaliza Urais wake ambapo, Obama atarudi Hawaii alikokulia na
Michelle atabaki Washington na wanae, Malia na Sasha. Kwa sasa inadaiwa
kuwa wawili hao wanalala vyumba tofauti na baada ya Obama kutaka kuweka
mambo sawa wakati wa mapumziko yao ya Christmas huko Hawaii, mambo
yaligeuka vibaya kiasi cha kumfanya Obama arudi na wanae hao wawili wa
kike mjini Washington na kumwacha huko mkewe.
The
National Enquirer,lilisema ilipata taarifa hizo kutoka kwa watu wa
ndani waliokataa kutajwa majina yao. Hata hivyo vyombo vya habari vya
Marekani vimeipuuzia habari hiyo. Hata hivyo kila mmoja anakumbuka jinsi
the Enquirer lilivyousema ukweli kuhusu mgombea wa urais wa chama cha
Democratic, John Edwards kuwa alizaa na mfanyakazi wa kampeni yake.
Walau
gazeti hilo lilikuwa sahihi katika upande mmoja — Ni kweli Mrs Obama
alibaki Hawaii. Ikulu ya White House ikatoa maelezo haraka kuwa
kuendelea kwake kukaa kulikuwa ni zawadi ya birthday kutoka kwa mumewe.
‘Kama
una watoto unajua kuwa kumwambia mwenzi wako kuwa anaweza kukaa wiki
mbali na nyumbani ni zawadi kubwa,’ alisema msemaji wa Ikulu.
Tangu
Obama achaguliwe kuwa rais, vitabu viwili vilidai kuwa wanandoa hao
walikaribia kuachana katika miaka yao ya mwanzo huku Mrs Obama akienda
mbali zaidi kwa kuandaa nyaraka za taraka baada ya shughuli zake za
siasa kuonekana zinaharibu furaha yao ya nyumbani.
Mwaka
2009, mwandishi wa habari mkongwe wa Marekani, Richard Wolffe alidai
kuwa ndoa hiyo kidogo ivunjike miaka tisa iliyopita kutokana na msukomo
wa siasa wa Obama na familia yake kuyumba kifedha. ‘Walikuwa
wakizungumza kidogo na mapenzi yalipungua,’ aliandika Wolffe.
Kipindi hicho, Mrs Obama alikuwa ametoka kuwa mama— watoto wao Malia na Sasha wana miaka 15 na 12.
Mumewe
ambaye walikutana wakati wakifanya kazi kwenye kampuni ya sheria 1989,
alikuwa seneta wa Illinois aliyekuwa ameshindwa kwenye uchaguzi wa kiti
cha Congress. ‘Alichukia hatua ya kushindwa kwa mumewe kwenye kiti cha
Congress mwaka 2000 na ndoa yao iliyumba kipindi binti yao Sasha,
alipozaliwa,’ aliandika Wolffe.
First
Lady wa zamani wa Ufaransa, Carla Bruni aliandika kwenye kitabu chake
kuhusu alivyomuuliza Michelle maisha yalivyo akiwa ikulu kama mke wa
Obama. ‘Usiulize! Ni jehanamu. Siwezi kuvumilia!’ Mrs Obama anadaiwa
kumwambia Carla. Mrs Obama baadaye alikanusha kuwahi kusema hivyo.
Mwaka
2012, mwandishi wa masuala ya siasa Edward Klein alidai kuwa Obama
alikuwa amehuzunishwa mno na kufeli kwa ndoa yake na mwaka 2000 marafiki
zake walikuwa na wasiwasi kuwa alikuwa anafikiria kujiua. ‘Michelle
alikuwa amechukia kwasababu alimuonya mumewe asigombee uchaguzi wa
Congress ambao alishindwa,’ alisema Klein.
‘Wakati
wa siku hizo za giza zilizokuja baada ya kushindwa, alirudi kwa
Michelle kupata liwazo. Lakini Michelle hakuwa na mood ya kumhurumia,’
aliandika Klein, ambaye alidai kuwa Michelle alifikia hatua ya kuandaa
taraka.
By Daily Mail