Unaweza
kuwa unampenda sana, lakini yule unayempenda akawa haonyeshi mapenzi ya
dhati, yaani siku zote umekuwa ni mtu wa kulia hauna furaha katika
uhusiano ulionao, na kwa wakati huo unajitahidi kwa kila njia kuweka
mambo sawa ili mwenzio akuelewe ni kiasi gani unampenda ili abadili
mwenendo wa tabia yake, lakini bado habadiliki, unabaki kulia na kuumia
kila kukicha. Wakati mwingine ni vyema kukaa na kutafakari unaambiwa
unaweza kuumia sana pale utakapoachana na yule unayempenda lakini,
kumbuka kama ni mtu ambaye hana mwelekeo wa kuleta furaha katika
uhusiano wenu basi siku zote utabaki ukilia na kuteseka. MPENDE
AKUPENDAYE ILI UWE NA MAISHA YENYE FURAHA, |