BAADA ya kusoma makala yangu ya leo na kuzingatia nilichokiandika,
bila shaka utaanza kuiangalia ndizi kwa mtazamo tofauti na uliokuwa nao
hapo awali. Ndizi mbivu ni tunda maarufu sana duniani lakini ni watu
wachache wanaojua uwezo, faida na maajabu yaliyomo kwenye tunda hili.
Ndizi ina
aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama Sucrose,
Fructose na Glucose na vilevile ina kiasi kingi cha ufumwele (fibre)
ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.
Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza
na kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata nishati ya kufanyakazi ya
muda wa dakika 90 kwa kula ndizi mbili tu. Bila shaka ndizi ni tunda
muhimu sana kwa wanamichezo. Hata hivyo, nishati siyo faida pekee
unayoweza kuipata katika ndizi, ni tunda lenye uwezo pia wa kuponya na
kuzuia matatizo mengi ya kiafya:
MFAIDHAIKO WA AKILI (DEPRESSION)
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama Cha Afya ya Akili cha Taifa
(MIND) cha nchini Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la
mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tatizo hilo na kujisikia
vizuri baada ya kula ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba
ndizi ina kirutubisho kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina
fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na
mwenye furaha.
MATATIZO WAKATI WA HEDHI
Kama wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo
mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na
unaweza kuponywa. Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi, hurekebisha kiwango
cha sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.
UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA)
Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina ya chuma (iron), inaweza
kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upunguvu wa damu kwa sababu madini ya
chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.
SHINIKIZO LA DAMU
Tunda hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango kikubwa cha madini ya
potasiamu (potassium) na wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha
chumvi (sodium) hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na
tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.
Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya Mamlaka ya Dawa na Chakula ya
nchini Marekani, iwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi
nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari
ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.
NGUVU YA AKILI
Hivi karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule ya Twickenham nchini
Uingereza, walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu wakati
wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na wakati wa chakula
cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao. Utafiti unaonesha kuwa
potasiamu iliyojazana kwenye ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi
kuamsha uwezo wake wa kujisomea.
KASUMBA (HANGOVERS)
Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana
yake (hangover) ni kunywa ‘Milkshake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na
kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa na asali, hurejesha
kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu wakati maziwa hutuliza na
kurejesha maji kwenye mfumo wake.
Mbali na matatizo yaliyoelezwa hapo
juu, ndizi pia husaidia katika matatizo mengine mengi kama vile
kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya
tumbo, kuondoa asidi tumboni, kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo
ya moyo, n.k
Hivyo ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni bora, ukiilinganisha na
Tufaa (Epo (Apple), ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga mara mbili,
vitamin A na chuma mara tano na vitamini na madini mengine mara mbili
zaidi ya tufaa. http://manyandahealthy.blogspot.com
Sunday, January 19, 2014
MAAJABU YA NDIZI MBIVU NA UHUMIHIMU WAKE KATIKA AFYA YA BINADAMU, HUONDOA MFADHAIKO WA AKILI.
Unknown