Msichana
mrembo aishie Uingereza, aliyetajwa kwa jina la Sunshine Haye,
amejitokeza na kudai kuwa na ujauzito wa mkali wa ‘Skelewu’, Davido na
kwamba anatarajia watoto mapacha.
Kwa
mujibu wa Naijaxclusive mrembo huyo ambaye anatokea Caribbean mwenye
asili ya Jamaica pia amedai kuwa Davido alimpa ujauzito huo mwaka jana
(2013) wakati alipokuwa kwenye ziara yake nchini Uingereza.
Msichana
huyo mwenye umri wa miaka 23, amedai kuwa hivi sasa ujauzito huo
umefikisha miezi kati ya minne hadi mitano na kwa mujibu wa tweets zake
alizoandika mwaka jana anatarajia watoto mapacha. “Twins!! I think I’m
gonna pass out.” Ni moja kati ya tweets za mrembo huyo.
Hata
hivyo, watu wa karibu wa Davido walipozungumza na mtandao huo
walikanusha taarifa hizo na kudai kuwa hawafahamu chochote kuhusu hilo.
Lakini camp ya mrembo huyo imesisitiza kuwa taarifa hizo ni za ukweli na kwamba watakuwa tayari kutoa vielelezo kuthibisha hilo.
Hii
si mara ya kwanza kwa msichana kujitokeza na kudai kuwa na ujauzito wa
Davido, July mwaka jana msichana mmoja Kenya alijitokeza na kuwaambia
waandishi wa habari kuwa alikuwa na ujauzito wa Davido, lakini mwisho wa
siku iligundulika kuwa taarifa hizo hazikuwa na ukweli wowote.