Tuesday, January 21, 2014

SYRIA YATUHUMIWA KUUA WAFUNGWA 10,000 TANGU KUANZA HARAKATI ZA KUMPINDUA RAIS BASHAR AL-ASAAD.

SYRIA_8c0cb.jpg
RIPOTI iliyotolewa na viongozi watatu wa zamani wa mashitaka ya uhalifu wa kivita inasema kwamba kuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kuwa Syria imewatesa na kuwaua karibu wafungwa 10,000 tangu kuanza harakati za kumpinga Rais Bashar Al-Asaad.


Wachunguzi walipekua maelfu ya picha za wafungwa waliokufa zilizotolewa nchini Syria na mpiga picha mmoja wa jeshi aliyetoroka kazi.

Wanasema miili mingi ilikuwa imekonda na mingine mingi kupigwa na kunyongwa.

Mmoja wa waandaaji wa ripoti hiyo, Professa Geoffrey Nice, aliambia BBC kuwa wingi na uhakika wa ushahidi uliotolewa unaonyesha wazi kuwa Serikali ilihusika katika ukatili huo.

Uchunguzi huo ulifadhiliwa na Serikali ya Qatar inayowaunga mkono waasi wa Syria. BBC imejaribu mara kadhaa kupata majibu ya Serikali ya Syria kuhusu madai hayo lakini Serikali haijatamka lolote. (J.M)

Madai kuwa wafungwa wamekuwa wakiteswa na kuuawa katika magereza ya Syria yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na wakereketwa wa haki za kibinadamu tangu maasi yaanze nchini humo miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo madai ya sasa yana upya fulani kwa njia ya kipekee.

Chanzo BBC Swahili
Habari hizi zina ushahidi kutoka kwa wandani wa Serikali wenyewe; mpiga picha wa kitengo cha jeshi cha polisi aliyetoroka kazi amewasilisha maelfu ya picha ambazo alipiga kabla ya kutoroka.


Na wachunguzi wa kimataifa, waliokuwa viongozi wa mashtaka sasa wanaamini kuwa picha walizoona za miili iliyoharibiwa vibaya, iliyopewa nambari na kupigwa picha mara kadhaa, ni ushahidi wa kuaminika.

Zaidi ya miili 11,000 ilipigwa picha ingawa bado kuna wasiwasi kuwa kuna maelfu ya watu ambao walizuiliwa magerezani lakini sasa hawajulikani waliko.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →