Mkutano wa kusaka amani Syria utaendelea bila Iran
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameufuta mwaliko aliokuwa
ameutoa kwa Iran kushiriki katika mazungumzo ya amani ya Syria ambayo
yanatarajiwa kuanza kesho nchini Uswisi.
Uamuzi huo
wa Ban Ki-moon ulifikiwa baada ya Iran kutupilia mbali mashariti
yaliyokuwa yakiambatanishwa na mwaliko huo. Msemaji wake Martin Nesirky
amesema Ban Ki-moon ameubatilisha mwaliko kwa Iran, baada ya nchi hiyo
kukiuka yale waliyokubaliana.
''Katibu mkuu amehuzunishwa sana
na tangazo lililotolewa na Iran, ambalo ni kinyume kabisa na ahadi
iliyokuwa imetolewa, na anaendelea kuitolea wito nchi hiyo kuunga mkono
maazimio ya mkutano wa Geneva.'' Amesema Nesirky.
Mwaliko huo
uliotolewa ghafla juzi jioni haukudumu hata kwa saa 24, na ulikuwa
umesababisha mtafaruku mkubwa, huku upinzani nchini Syria ukitishia
kujitenga kabisa na mkutano wa kesho iwapo Iran ambayo ni mshirika
mkubwa wa rais Bashar al-Assad ingeshiriki kwenye meza ya mazungumzo.
Iran 'ilikiuka' ahadi zake
Umoja wa Mataifa umesisitiza kwamba waziri wa mambo ya nchi za nje wa
Iran Javad Zarif alikuwa amemhakikishia Ban Ki-moon kwamba anaelewa
vilivyo, na anaunga mkono lengo la mazungumzo ya amani ambalo ni kuunda
serikali ya mpito.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Javad Zarif
Lakini kabla ya kubatilishwa kwa mwaliko huo kwa Iran, balozi wa nchi
hiyo kwenye Umoja wa Mataifa Mohammad Khazaee alikariri msimamo wa
serikali yake, kwamba ikiwa kushiriki kwake katika mazungumzo
kunafunganishwa na masharti ya kukubali maazimio ya mkutano wa kwanza wa
Geneva, basi haitakwenda katika mkutano wa pili.Umoja wa Mataifa
umesema katibu mkuu Ban alifanya mashauriano na Marekani na Urusi kabla
ya kufuta mwaliko kwa Iran.
Marekani imesema inazo taarifa
kutoka ndani ya serikali ya mjini Damascus, kwamba serikali hiyo inataka
suluhisho la amani kwa mgogoro unaoendelea nchini humo.
Ingawa
mkutano wa Montreux ambao pia umepachikwa jina la Geneva II unaanza
kesho, wajumbe wa serikali ya Syria na wa upinzani wataanza kuzungumza
Ijumaa. Bado vipo vizingiti vikubwa kwa mazungumzo hayo, ambavyo
vimedhihirishwa na mpasuko wa ndani kwa upande wa waasi, msimamo mkali
wa rais Bashar al-Assad, na kuendelea kwa ghasia ambazo zinavuka mpaka
na kuingia katika nchi jirani.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lavrov
Mkusanyiko wa kiitifaki
Urusi ambayo ni mshirika wa serikali ya Syria na mmoja wa waandaaji wa
mkutano wa Geneva, imesema litakuwa kosa kubwa kutoishirikisha Iran
katika mkutano huo. Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Moscow
muda mfupi uliopita, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei
Lavrov amesema bila Iran mkutano wa kesho hautakuwa na chochote zaidi ya
utaratibu wa kiitifaki. Iran nayo imesema ina mashaka juu ya mafanikio
ya mkutano huo.
Muungano mkuu wa upinzani dhidi ya serikali ya
rais Bashar al-Assad umesema utakwenda kwenye mkutano huo utakaofanyika
katika mji wa Montreux, lakini kundi jingine kubwa lijulikanalo kama
Baraza la Kiataifa la Syria limejitenga na mazungumzo hayo, likishikilia
msimamo wake wa kutoshiriki mazungumzo yoyote hadi pale rais Assad
atakapokuwa ameondoka madarakani.
Kwa mujibu wa takwimu za
shirika la kuchunguza haki za binadamu nchini Syria ambalo lina makao
yake nchini Uingereza, watu takribani 130,000 wamekwishauawa katika vita
wenyewe kwa wenyewe vya Syria ambavyo
Tuesday, January 21, 2014
KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA AFUTA MWALIKO WA IRAN.
Unknown